Idara inayosimamia haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imeratibu mambo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya mazazi ya Mtume mtukufu na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Idara inayosimamia haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imeratibu mambo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya mazazi ya Mtume mtukufu na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Kiongozi wa idara Sayyid Aqiil Twaif amesema “Hakika idara iliandaa mambo mbalimbali katika maadhimisho ya Mtume mtukufu na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s), ikiwa ni pamoja na kuweka chupa za mauwa juu ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya haram tukufu, sambamba na kupokea mazuwaru wanaokuja kutembelea malalo hiyo takatifu kwa kuwapa manukato”.

Akafafanua kuwa, Idara inamajukumu mengi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa majukumu yake ni kusafisha haram, kupuliza marashi, kuhudumia mazuwaru, kuweka vitabu vya dua na ziara kwenye kabati za vitamu, kutandika mazulia mapya na mengineyo.

Akaongeza kuwa “Tuna watumishi maalum amboa husafisha dirisha la kaburi, pambo la dhahabu (Twarima), mlango wa qibla, dirisha na Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) na Sardabu zilizopo ndani ya haram tukufu kwa kutumia vifaa maalum”.

Akasisitiza kuwa, watumishi wa idara yetu wanadumisha usafi kwenye maraya na eneo lote la haram tukufu, aidha wanasafisha kuta, kashi-karbalaa, kubadili pazia za kwenye milango katika kila tukio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: