Idara ya Fatuma binti Asadi inaadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Idara ya Fatuma binti Asadi inayohusika na masomo ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya, imeadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Kiongozi wa Idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Idara imeadhimisha mazazi ya (Swadiqaini) wakweli wawili (a.s) katika kituo cha Sidri, kwa kufanya safari ya mapumziko iliyohusisha wanafunzi na walimu wa idara”.

Akaongeza kuwa “Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na mmoja wa mahafidh wa idara, ukafuata muhadhara kutoka kwa mmoja wa walimu aliyeongea kuhusu historia wa (Swadiqaini) wakweli wawili (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Hafla imehusisha usomaji wa tenzi, qaswida na mashindano ya Qur’ani ya mtu mmoja mmoja na vikundi, washindi wakapewa zawadi katika mazingira ya shangwe na furaha”.

Kwa mujibu wa Mussawi “Hafla za matukio ya kidini ni jambo ya kijamii ambalo hupewa umuhimu mkubwa, aidha ni kuhuisha mafundisho ya Dini na kumfuata Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: