Ataba imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya (Swadiqaini) wakweli wawili katika ukanda wa kijani.

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya (Swadiqaini) wakweli wawili (a.s) katika ukanda wa kijani kusini mwa mkoa wa Karbala.

Rais wa kitengo cha ukanda wa kijani kibichi chini ya Atabatu Abbasiyya Huquqi Naasir Husseini amesema “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s) kwenye uwanja wa Rasuulu-A’adham uliopo katika ukanda wa kijani kusini mwa mkoa wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Hafla imehudhuriwa na kundi kubwa la familia zinazotembelea eneo hilo, sambamba na ushiriki wa wasomaji wa mashairi na qaswida zinazohusu furaha ya maadhimisho haya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: