Katika nchi ya Komoro.. kitengo cha Habari na utamaduni kimeadhimisha mazazi ya (Swadiqaini) wakweli wawili (a.s).

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) katika nchi ya Komoro.

Maadhimisho hayo yamesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Muwakilishi wa Markazi katika nchi ya Komoro Shekhe Habibu Waali, amefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Mtume mtukufu na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Katika hafla hiyo umetolewa muhadhara kuhusu utukufu wa Mtume (s.a.w.w) mbele ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Markazi kupitia muwakilishi wake Shekhe Habibu Waali imeshiriki kwenye hafla mbalimbali za kuadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w) zilizo andaliwa na taasisi zingine katika nchi hiyo, kwa lengo la kujenga ushirikiano na ukaribu baina ya waislam, kwa mujimu wa Shekhe Shimri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: