Kitengo cha Maqaam ya Imamu Alhujjah (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya, husoma Dua ya Nudba kila asubuhi ya siku ya Ijumaa.
Kila asubuhi ya siku ya Ijumaa husomwa Dua ya Nudba katika mazingira tulivu ya kiibada, idadi kubwa ya mazuwaru hushiriki kwenye dua hiyo.
Watumishi wa Maqaam huweka mazingira rafiki kwa ajili ya usomaji wa Dua hiyo, ikiwa ni pamoja na kuandaa sehemu maalum ya kufanyia ibada, kuandaa msomaji wa Dua pamoja na mambo mengine.