Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani kila siku kwa jina la (katika uwanja wa Qur’ani).

Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani kila siku kwa jina la (Katika uwanja wa Qur’ani) ndani ya sardabu ya Imamu Hussein (a.s) chini ya usimamizi wa idara ya Qur’ani.

Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shami amesema “Kikao kitafanyika saa nne na nusu asubuhi kila siku, kwa lengo la kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Lengo la ratiba hii sio kusoma Qur’ani pekeyake, bali ni kusahihisha usomaji wa washiriki, kufafanua baadhi ya hukumu za tajwidi, kutafsiri baadhi za aya zinazohusu hukumu za kisheria au muongozo wa kimaadili”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Shami “Idara hufanya matukio yanayohusu Qur’ani mara nyingi, kama vikao vya usomaji wa Qur’ani, kutembelea maeneo maalum na kufundisha Fiqhi, Aqida na Akhlaqi, aidha tunamfundisha mwanamke namna ya kushikamana na utamaduni wa dini na Qur’ani tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: