Idara ya Fatuma binti Asadi imetangaza kuanza kwa usajili wa semina ya Manaahil Furqaan kwa njia ya mtandao.

Idara ya Fatuma binti Asadi ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuanza kusajili watakao shiriki kwenye semina ya (Manaahil Furqaan) kwa njia ya mtandao kuhusu hukumu za usomaji.

Semina itakuwa inafanywa siku ya Jumanne katika kila wiki, kuanzia saa 4:00 hadi saa 5: 00 asubuhi.

Idara imetoa vigezo na masharti ya kushirki kwenye semina hiyo, miongoni mwa vigeno mshiriki hatakiwi kuwa na chini ya umri wa miaka 15 na sio zaidi ya miaka 40, awe anaweza kusoma vizuri japo kwa asilimia 60.

Mshiriki anatakiwa ahudhurie darasa kwa njia ya mtandao kuanzia mwanzo wa kipindi hadi mwisho katika siku zote za semina, asipo hudhuria mara mbili anatolewa kwenye ushiriki, na anatakiwa azingatie na kutekeleza maagizo yote atakayopewa.

Mshiriki anatakiwa kutuma rekodi yake ya sauti akisoma surat Alfaatiha na Tauhidi kwenye namba zifuatazo (07714593468 – 07602455278), tambua kuwa siku ya mwisho ya kupokea rekodi za washiriki ni tarehe (10/10/2023m).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: