Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imepokea wanafunzi wa Maahadi ya wahadhiri kufuatia kuingia mwaka mpya wa masomo.
Kiongozi wa idara bibi Taghridi Tamimi amesema “Kufuatia kuingia mwaka mpya wa masomo, Idara imepokea wanafunzi 70 wa darasa la awali kwa ajili ya kuwaandaa waingie hatua inayofuata”.
Akaongeza kuwa “Maahadi imegawa selebasi za masomo kwa wanafunzi wapya, na imeandaa masomo kwa kutumia mfumo mpya unaowezesha kujenga uwezo wa washiriki”, akafafanua kuwa “Maahadi inafundisha masomo tofauti kama vile Qur’ani, Sira, Sauti, Maqamaati, Nagham na namna ya kuandika tafiti na mihadhara”.
Maahadi imejikita katika kuandaa wahadhiri mwenye uwezo mkubwa na uwelewa mzuri kuhusu Ahlulbait (a.s), na kuongeza uwezo wao wa kupambana na changamoto wanazokutana nazo kwa sasa na baadae.