Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inawatahini waliohifadhi juzu la kwanza la msahafu mtukufu.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya limewatahini wanafunzi waliohifadhi juzu la kwanza katika msahafu mtukufu.

Wanafunzi (16) wa kuhifadhi Qur’ani kutoka tawi la Baabil ndio waliotahiniwa.

Idara ya Maahadi imetoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri na imeonyesha kufurahishwa na maendeleo mazuri ya wanafunzi katika kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Idara ya Maahadi imehimiza kuendelea kuhifadhisha Qur’ani tukufu na imewashajihisha wanafunzi waendeleze juhudi ya kuhifadhi majuzuu yaliyobaki hadi wamalize kuhifadhi kitabu chote cha Mwenyezi Mungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: