Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na usomaji wa Qur’ani Tartiil kila siku ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Usomaji huo unasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Kikao cha usomaji wa Qur’ani ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kimepata ushiriki mkubwa kutoka kwa wasomaji wa Qur’ani, akiwemo Thaamir Twaahir na mahafidhi wawili ambao ni Farajawi na Mustwafa Saaduni.
Usomaji wa Qur’ani ni sehemu ya harakati ya Majmaa-Ilmi inayolenga kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa waislamu.
Usomaji wa Qur’ani tukufu unalenga kusaidia taasisi za Qur’ani zinazohifadhisha na kufundisha usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.