Kitengo cha uhusiano kinafanya warsha kwa watumishi wa Ataba zaidi ya mia moja.

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kinafanya warsha ya kutambulisha Ataba, ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo watumishi wapya, program hii imewalenga watumishi wa kitengo cha kulinda nidham.

Mkufunzi wa warsha Sayyid Mustwafa Arsani amesema “Wakufunzi wa kitengo cha mahusiano wamefanya warsha ya kutambulisha Atabatu Abbasiyya na mfumo wa uongozi wake kwa watumishi wapya zaidi ya mia moja”.

Akaongeza kuwa “Miongoni mwa malengo ya warsha ni kuwatambulisha miradi ya kimkakati inayofanywa na Atabatu Abbasiyya, iliyoanzishwa chini ya malengo ya maendeleo endelevu”.

Akasema: “Warsha itadumu kwa muda wa wiki nzima, inahusisha mihadhara ya kifiqhi, Akhlaq, Sira ya Mtume (s.a.w.w) na Ahlulbait wake watakasifu (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: