Majmaa-ilmi inafanya harakati ya Qur’ani katika vyuo vikuu vyote vya Iraq.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imeanzisha harakati ya ufundishaji wa Qur’ani kwenye vyuo vikuu vyote vya Iraq.

Harakati hiyo inasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Mkuu wa idara ya harakati za Qur’ani Sayyid Wahaji Al-Abadi amesema “Ratiba mpya imeanza kutekelezwa katika chuo kikuu cha Misaan, tumefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani kwa kushirikiana na kitivo cha malezi”.

Akaongeza kuwa “Vikao hivi ni sehemu ya mkakati unaolenga tabaka la wanafunzi wa chuo kwa kuwajengea mafungamano imara na Qur’ani pamoja na kizazi kitakatifu”.

Akabainisha kuwa “Ratiba imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi na walimu”, akasema: “Mradi huu unasimamiwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi kupitia Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: