Tawi la kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya limepata muitikio mkubwa kwenye maonyesho ya vitabu.
Mshiriki wa maonyesho hayo Shekhe Twaahir Alghanimi amesema “Tuna vitabu vingi vilivyo chapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye kiwanda cha Alkafeel, vitabu hivyo vinamaudhui za kitamaduni na maarifa tofauti na vinauzwa kwa bei nafuu”.
Akaongeza kuwa “Tumevutia watu kutoka mataifa tofauti, kwani tunavitabu vilivyo andikwa kwa lugha ya kiengereza na vitabu vya watoto”.
Akaendelea kusema “Vitabu vyetu vinaubora mkubwa, vinakaratasi imara na herufi nzuri zinazosomeka kwa urahisi jambo ambalo linavutia wasomi na watafiti kwa ujumla”.