Atabatu Abbasiyya inashiriki kwenye maonyesho ya vitabu ikiwa na machapisho zaidi ya (750).

Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu yanayosimamiwa na Atabatu Kadhimiyya ikiwa na zaidi ya machapisho (750) ya aina mbalimbali.

Kiongozi wa tawi la Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad A’araji amesema “Atabatu Abbasiyya imeshiriki kupitia kitengo cha Habari na utamaduni, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu na kamati kuu ya kuhuisha turathi, ikiwa ni sehemu ya kushiriki kwenye maonyesho ya ndani na nje”.

Akaongeza kuwa “Tawi la Atabatu Abbasiyya inazaidi ya machapisho (750) ya aina mbalimbali” akabainisha kuwa: “Machapisho yote yaliyopo kwenye tawi letu yameandikwa na kuchapishwa na Atabatu Abbasiyya”.

Tawi la Atabatu Abbasiyya linasifika kwa kuwa na vitabu vya aina tofauti vyenye maudhui muhimu katika uwanja wa Dini, utamaduni na maarifa ya kitaifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: