Tamko kutoka ofisi ya Sayyid Sistani kuhusu mashambulizi yanayoendelea ukanda wa Gaza.

Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani imetoa tamko kuhusu mashambulizi yanayoendelea kila mahala katika ukanda wa Gaza nchini Palestina.

Ifuatayo ni nakala ya tamko:

Ukanda wa Gaza unashambuliwa mfululizo kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijapata kushuhudiwa, hadi sasa zaidi ya raia elfu sita wasiokua na hatia wameuwawa au kujeruhiwa, huku idadi kubwa ya watu wakihama makazi yao na nyumba nyingi zikiwa zimebomolewa, kila sehemu inashambuliwa na hakuna mahala salama pakujificha.

Wakati huohuo jeshi la wavamizi limeweka mzingiro mkali katika ukanda wa Gaza, hivi karibuni limewakatia maji na kuzuwia kupelekewa chakula, dawa na mahitaji mengine ya lazima kwa uhai wa mwanaadamu, hakika raia wanahali ngumu sana, kana kwamba maadui wanataka kulipiza kisasi kwa raia wasiokuwa na hatia, kufuatia kushindwa kwao kwenye mashambulizi ya hivi karibuni.

Unyama huo unafanywa huku dunia ikiwa imefumba macho na kuziba masikio, bali jambo la kusikitisha zaidi bado kuna nchi zinaunga mkono mauwaji hayo kwa madai kuwa ni haki ya kujilinda.

Hakika ni wajibu kwa dunia nzima kukemea mauwaji haya na kuhakikisha wavamizi wanaacha kuuwa raia wa Palestina.

Njia pikee ya kuleta amani na usalama kwa raia hawa watukufu na kuondoa mateso -yaliyodumu kwa miongo saba-, ni kuondoka wavamizi katika ardhi yao, bila kuondoka kwa wavamizi hao (mazayuni) mapambano yataendelea na watu wataendelea kupoteza maisha zaidi.

Hakuna hila wala nguvu ispokua kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: