Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini ametembelea tawi la Ataba tukufu kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya tisa yanayosimamiwa na Atabatu Kadhimiyya.
Muheshimiwa katibu mkuu ameangalia mambo yanayo onyeshwa na tawi la Ataba tukufu kwenye maonyesho hayo.
Aidha amesikiliza maelezo kuhusu vitabu, majarida na machapisho mbalimbali yaliyopo kwenye maonyesho hayo kutoka kwa washiriki.
Akasisitiza umuhimu wa kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Ataba wanaoshiriki kwenye maonyesha kama haya, sambamba na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na wahudumu wa tawi hilo.
Atabatu Abbasiyya imewakilishwa na kitengo cha habari na utamaduni, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu na kamati kuu ya kuhuisha turathi, huku wakiwa na vitabu na machapisho mbalimbali zaidi ya (750).