Sayyid Swafi amesisitiza kuwa: Iraq inauwezo mkubwa wa kuendeleza taifa.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, Iraq inarasilimali nyingi zinahitaji kutumiwa kwa maendeleo ya taifa, inawatu wenye uwezo wa kuleta maendeleo.

Ameyasema hayo alipokutana na Muheshimiwa mjumbe wa kamati ya mjadala wa kitaifa kuhusu nishati.

Kiongozi mkuu wa kisheria amesisitiza umuhimu wa kupanda miti, akafafanua ulazima wa kuwa na ukanda wa kijani kwenye kila mkoa, kwani jambo hilo linafaida kubwa na matokeo mazuri kwa binaadamu.

Akataja rasilimali nyingi zilizopo na zinahitaji kutumiwa, akasema taifa hili linawatu wenye uwezo wa kuleta maendeleo.

Aidha Muheshimiwa ametaja uzowefu wa Atabatu Abbasiyya kwenye sekta ya kilimo na mchango wake katika upatikanaji wa chakula hapa nchini, akabainisha kuwa Atabatu Abbasiyya imetumia jua kama njia kuu ya kupata umeme kwenye miradi yake.

Rais wa kamati ya kuendesha mjadala wa kitaifa kuhusu nishati Dokta Jaasim Alfalahi amesema “Leo tumepata nasaha muhimu kutoka kwa Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria, aidha tumetambua mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye miradi ya kimaendeleo, na tumewasilisha maoni yetu yanayolenga kutambua mchango wa jamii katika kufanyia kazi nishati mpya na kuboresha uwezo wa upatikanaji wa nishati ya umeme”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: