Majmaa-Ilmi imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa kupitia ratiba ya kila wiki ya (Arshu-Tilawah).

Sayyid Hasanaini Shimri kutoka kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa-Ilmi amesema kuwa “Kituo kimeandaa ratiba ya usomaji wa Qur’ani ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, kupitia ratiba ya kila wiki ya (Arshu-Tilawah)”.

Akaongeza kuwa “Kikao hiki cha usomaji wa Qur’ani ni sehemu ya kumpongeza mwanafunzi wa mradi Hussein Ali Alhajaar kwa kuwa mshindi wa pili kwenye mashindano ya balozi wa Qur’ani yaliyofanyika Masjidi-Kufa”.

Akaendelea kusema kuwa “Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inashajihisha wanafunzi wake kuhifadhi Qur’ani na kujiandaa kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: