Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, ameshiriki kwenye kikao cha makatibu wakuu wa Ataba takatifu, kilichafanyika katika Atabatu Alkadhimiyya.
Wengine walioshiriki kikao hicho ni katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya Sayyid Issa Khurasani, katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Ustadh Hassan Al-Abaiji, katibu mkuu wa Atabatu Askariyya Dokta Muhammad Qassim na mwenyeji wao katibu mkuu wa Atabatu Alkadhimiyya Dokta Haidari Hassan Shimri.
Katika kikao hicho wamejadili namna ya kushirikiana baina ya Ataba zao katika kila jambo linalohusu kuhudumia mazuwaru wa Maimamu watakasifu (a.s).
Aidha wameeleza mambo muhimu yanayofanywa na Ataba zao kwenye sekta ya uhandisi, ujenzi na utoaji wa huduma tofauti kwa mazuwaru watukufu.
Washiriki wote wa kikao hicho wamekubaliana kuimarisha ushirikiano, kwa lengo la kufikia malengo yao makuu ambayo ni kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu.