Kitengo cha habari kimetoa chapisho la (470) la jarida la Swada-Raudhatain.

Hivi karibuni kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa chapisho la (470) la jarida la Swada-Raudhatain, linaloandika kuhusu mafanikio ya Ataba tukufu na harakati za vitengo vyake.

Toleo hili linajumla ya kurasa (84) zilizoandika matukio muhimu yaliyofanywa na Ataba tukufu pamoja na ripoti za vitengo mbalibali sambamba na kuangazia kongamano na tamasha za kidini na kitamaduni.

Jarida la Swada-Raidhatain huandika mafanikio yaliyofikiwa na Atabatu Abbasiyya pamoja na harakati za vitengo vyake, nalo ndio jarida la kwanza katika historia ya Ataba tukufu, huchapishwa na idara ya Habari za kuandikwa/ kitengo cha Habari.

Jarida hilo huandika mambo tofauti kwenye kurasa zake, jambo kubwa likiwa ni matukio muhimu yanayofanywa na vitengo vya Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: