Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha toleo la saba katika mfululizo wa tafiti za kidini kwa jina la (Dini, Elimu na Nafsi).
Kitabu hicho kimeandikwa na Sayyid Ahmadi Qutbi na kuchapishwa na kituo cha tafiti za kiislamu chini ya kitengo.
Kitabu kinamaudhui nyingi, miongoni mwake kutafakari katika elimu ya Nafsi na Dini, umuhimu wa kuanzisha kitengo cha Elimu ya Nafsi cha kiislamu na misingi ya elimu hiyo, elimu ya uwelewa wa nafsi, elimu ya majukumu yake, elimu ya upeo wa nafsi na mwenendo wake, afya ya nafsi na kutengua baadhi ya fikra katika elimu ya nafsi ya kimagharibi.
Hiki ni kitabu cha kisasa katika elimu hii muhimu, kinawafaa walimu, watafiti, wanafunzi wa hauza, wanafunzi wa vyuo vikuu na kila anaetaka kujua maudhui hii.
Kwa maelezo zaidi fungua link ifuatayo: https://www.iicss.iq/?id=3689
Link ya kituo cha kiislamu cha tafiti za kimkakati: https://t.me/iicss