Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaangalia maendeleo ya mradi wa kuhifadhi Qur’ani katika mkoa wa Baghdad.
Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu/ tawi la Baghdad Sayyid Nabiil Saaidi amesema “Maahadi inaendelea na ratiba ya kukagua semina za kuhifadhisha Qur’ani zinazofanywa kwenye maeneo tofauti ndani ya mji mkuu wa Baghdad, kwa lengo la kutambua kiwango walichofikia wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani”.
Akaongeza kuwa “Wanafunzi wamepiga hatua kubwa kwa kuhifadhi juzuu kadhaa za kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, chini ya walimu bobezi wanaojua mbinu zinazo msaidia mwanafunzi kuhifadhi haraka na kudhibiti alicho hifadhi katika akili yake”.
Maahadi inafanya kazi kubwa ya kufundisha Qur’ani tukufu katika jamii, kupitia mradi wa kufundisha na kuhifadhisha Qur’ani tukufu.