Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya semina za kuwajengea uwezo watumishi wake.

Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina za kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo cha maelekezo ya kinafsi, kimalezi na idara ya ufuatiliaji.

Semina imefunguliwa kwa muhadhara uliotolewa na mkuu wa kitengo cha maelekezo ya kimalezi Dokta Husaam Ubaidi na mkuu wa idara ya ufuatiliaji Dokta Ayadi Taki wenye anuani isemayo (Umuhimu wa malezi katika vyuo vikuu).

Muhadhara ulikuwa na vipengele tofauti, miongoni mwa vipengele hivyo ni uwelewa wa malezi na umuhimu wake katika elimu, malezi kamili na mazuri, umuhimu wa maelekezo ya kimalezi katika vyuo vikuu.

Washiriki wa semina hii wanafundishwa mambo mbalimbali yanayo lenga kuwajengea uwezo katika vitu tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: