Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na vikao vya kusoma Qur’ani kila wiki katika wilaya ya Hamza mashariki.
Usomaji wa Qur’ani unasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hamza mashariki chini ya Majmaa.
Usomaji wa Qur’ani unafanywa kila siku ya Jumanne kwa ushiriki wa wakazi wa wilaya hiyo katika mazingira tulivu, vikao hivyo huongozwa na wasomi wafuatao, Muhammad Shaakiri Khaliil, Muhammad Nabiil Jawaad, Maajid Abduridha na Bahaa Subhi Khaliil.
Inahusisha pia kusahihisha usomaji wa aya za Qur’ani tukufu kwa washiriki wa kikao vya usomaji wa Qur’ani.