Idara ya Fatuma binti Asadi inayohusika na masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kutoa mihadhara katika semina ya (Manaahil-Furqaan) ya kimtandao inayofanywa kila wiki.
Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Watumishi wa idara wameanza kutoa mihadhara kupitia semina isemayo (Manaahil-Furqaan) ya kimtandao inayofanywa kila wiki chini ya walimu bobezi, wameanza kueleza umuhimu na utukufu wa Qur’ani kupitia hadithi za Ahlulbait (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Washiriki wamepewa mtihani wa kusoma surat Fat-ha, kwani hiyo ni rura muhimu katika ibada ya swala kisha ukatolewa muhadhara wa kwanza kuhusu hukumu za usomaji wa Qur’ani na matamshi ya herufi”.
Akaendelea kusema “Idadi ya washiriki ni (60) kutoka mikoa tofauti ya Iraq”, akasema “Idara inafanya harakati zake kwa kuhudhuria wahusika mubashara au kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuitumikia jamii”.