Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya, imefanya muhadhara wa kifiqhi kwa watumishi wake.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Muhadhara wa kifiqhi umeandaliwa na Maahadi katika ofisi ya Najafi kwa watumishi na walimu, wamefundishwa kuhusu taqlidi na umuhimu wake kwa mtu anayewajibikiwa na sheria, iwapo ibada zake zisipofanywa chini ya uwanja wa taqlidi”.
Akaongeza kuwa “Uendeshaji wa masomo haya katika Maahadi ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya, unaolenga kuwafundisha mambo ya halali na haram kutoka ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu na sunna za Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.
Maahadi huendesha warsha na kutoa mihadhara kwa watumishi wake kila wakati, kwa lengo la kujenga uwezo wao kielimu na kuwapa uwelewa utakao wasaidia katika Maisha yao.