Wataalam wa Alkafeel wanafanya semina ya (76) kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya.

Wataalam wa kitengo cha uokozi katika Atabatu Abbasiyya wanafanya semina ya (76) kwa watumishi wa Ataba tukufu, semina hiyo imepewa jina la (Mashahidi wa Gaza).

Kiongozi wa idara ya mipango na mafunzo Sayyid Muhammad Aamiri amesema kuwa “Semina imedumu kwa muda wa siku tano, imehusisha watumishi wa kitengo cha kulinda nidham, kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili na kitengo cha Maqaam tukufu”.

Akaongeza kuwa “Semina imejikita katika kueleza matukio ya kivita, hali ya kukosa hewa, njia za kuamiliana na mtu aliyevunjika viungo, majeruhi na mambo mbalimbali kuhusu namna ya kuokoa Maisha ya mtu”.

Wataalam wa Alkafeel hutoa mafunzo ya uokozi kupitia semina na warsha mbalimbali kwa ajili ya kujipanga na kuokoa Maisha ya mazuwaru wanaoweza kupata matatizo ya kiafya wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu na hata katika siku za kawaida.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: