Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha maandalizi ya kongamano la Daaru Rasuul la kimataifa awamu ya tatu litakalo fanyika Alkhamisi ya kesho.
Kongamano hilo limeandaliwa na taasisi ya Daaru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) chini ya kauli mbiu isemayo (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anawasomea nyaraka takatifu) na anuani isemayo (Historia ya Mtume katika vitabu vya tafsiri), kongamano litadumu kwa muda wa siku mbili.
Awamu ya tatu itakuwa na washiriki wa ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kusoma historia ya Mtume katika misingi ya kielimu.