Leo asubuhi limefanywa kongamano chini ya kauili mbiu isemayo (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anawasomea nyaraka takatifu) na anuani isemayo (Historia ya Mtume katika vitabu vya tafsiri).
Rais wa Daru Sasuulul-A’dham Dokta Aadil Nadhiri amesema “Kongamano linalenga kutambulisha utukufu wa Mtume (s.a.w.w) aliyeweza kubadilisha umma kupitia Qur’ani takatifu”.
Akaongeza kuwa “Historia ya Mtume na utukufu wake (s.a.w.w) vinatakiwa vijulikane” akaongeza kuwa “Inatakiwa kumuelezea Mtume (s.a.w.w) kwa kiwango kinacho hitajika katika zama hizi”.
Akasema “Utukufu wa Mtume (s.a.w.w) unaelezewa na aya za Qur’ani tukufu”.