Mtafiti kutoka chuo kikuu cha Mustanswariyya ameongea kuhusu vita ya Hunain kwa kutumia vitabu vya tafsiri.

Mtafiti kutoka chuo kikuu cha Mustanswariyya Hanani Shihabu Ahmadi, ameongea kuhusu vita ya Hunaini katika vitabu vya tafsiri.

Amewasilisha utafiti wake katika kikao cha jioni cha kongamano la tatu la Rasuulul-A’dham (s.a.w.w), chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, linalofanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anasoma nyaraka takatifu) na anuani isemayo (Historia ya Mtume katika vitabu vya tafsiri).

Utafiti uliopewa jina la (Vita ya Hunain katika vitabu vya tafsiri) umeonyesha kuwa, hiyo ni miongoni mwa vita muhimu katika historia ya kiislamu, kutokana na kuonyesha jambo adhimu la ukubwa wa Imani na msimamo wa waislamu pamoja na hali ngumu waliyokuwa nayo.

Mtafiti akasema kuwa vitabu vya tafsiri vimeonyesha umuhimu wa vita hiyo, na jinsi waislamu walivyo fanya Subira kwa ajili ya kutafuta ushindi.

Akabainisha kuwa sio vitabu vya tafsiri peke yake vilivyo Andika umuhimu wa vita hiyo katika uislamu, hata vitabu vya historia vimeandika umuhimu wake na jinsi ilivyokuwa na athari kwa waislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: