Kuanza ratiba ya siku ya pili katika kongamano la Daaru Rasuulul-A’dham la kimataifa awamu ya tatu.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza utekelezaji wa ratiba katika siku ya pili ya kongamano la Daaru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) la kimataifa awamu ya tatu.

Kongamano hilo linasimamiwa na kitengo cha Habari na utamaduni katika Ataba tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anasoma nyaraka takatifu) na anuani isemayo (Historia ya Mtume katika vitabu vya tafsiri).

Katika siku ya pili ya kongamano hilo, amehudhuria mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami, wajumbe wa kamati kuu ya Ataba, marais wa vitengo na baadhi ya viongozi wa kidini na kisekula.

Kikao kimefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na msomaji wa Majmaa Ilmi ya Qur’ani katika Atabatu, Sayyid Ammaari Alhiliy.

Ratiba ya asubuhi imeongozwa na Dokta Taqi, shughuli zake zimefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), huku awamu nyingine ikifanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) katika Ataba tukufu, chini ya usimamizi wa Dokta Najmu Abdullah Mussawi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: