Atabatu Abbasiyya imeanza kutekeleza ratiba ya jioni katika siku ya pili ya kongamano la Daaru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) awamu ya tatu.
Kongamano hilo linasimamiwa na kitengo cha Habari na utamaduni katika Ataba, chini ya kauli mbiu isemayo (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anasoma nyaraka takatifu) na anuani isemayo (Historia ya Mtume katika vitabu vya tafsiri) na litadumu kwa muda wa siku mbili.
Kikao cha jioni kimehudhuriwa na viongozi wengi wa Ataba tukufu pamoja na viongozi wa kihauza na kisekula.
Kikao cha jioni kimesimamiwa na Dokta Walidi Abdulhamiid Khalf ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) na kimejikita katika mambo ya kiitikadi na kifiqhi, huku mada zilizowasilishwa kwa lugha ya kiengereza zikitolewa katika ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) ndani ya Ataba na kusimamiwa na Dokta Riyaadh Twariq Al-Amiidi.