Idara ya Fatuma binti Asadi inaendelea na ratiba ya kitablighi ya (Ulizeni wanaojua).

Idara ya Fatuma binti Asadi katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na ratiba ya kitabligh ya kila wiki iitwayo (ulizeni wanaojua).

Kiongozi wa idara ya Fatuma binti Asadi katika Atabatu Abbasiyya bibi Fatuma Mussawi amesema “Ratiba imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na ripoti kwa ufupi kuhusu shughuli zinazofanywa na Ataba katika jamii kwa ujumla”.

Akaongeza kuwa “Ratiba ilikuwa na uwasilishaji wa masomo ya kifiqhi katika mada tofauti, ikiwemo mada ya eda ya talaka na eda ya kufiwa pamoja na mambo mengine tofauti, na kujibu maswali mbalimbali kuhusu historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) sambamba na kutambulisha yaliyotufikia kutoka kwa maimamu watukufu”.

Akaendelea kusema “Ratiba ilikuwa na kipengele cha kutambulisha kitabu cha mmbora wa wanawake ulimwenguni bibi Zahara (a.s), sambamba na kipengele cha watoto kupitia ratiba ya (uwanja wa watoto)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: