Akasema kuwa “Kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya juhudu kubwa kufikia kiwango cha juu kielimu na kutoa madaktari bora, akasisitiza kuwa ufundishaji unategemea mbinu za kisasa”.
Akaongeza kuwa “Kuna muitikio mkubwa wa wanafunzi kutokana na kuwepo kwa mfumo bora wa ufundishaji na maabara ya kisasa yenye mahitaji yote ya lazima kwa mwanafunzi”.
Akaendelea kusema: “Chuo kimeajiri walimu bora na wabobezi katika fani zao kutoka ndani na nje ya Iraq”.