Kwa watumishi wake.. Idhaa ya Alkafeel inatoa muhadhara wenye anuani isemayo (Utukufu wa elimu).

Idhaa ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya imetoa muhadhara wenye anuani isemayo (Utukufu wa elimu) kwa watumishi wa idhaa hiyo.

Kiongozi wa Idhaa bibi Baslam Rabii amesema “Muhadhara ni sehemu ya muendelezo wa ratiba ya kueleza aya tukufu za Qur’ani na riwaya zinazo himiza kutafuta elimu na umuhimu wa wanachuoni katika umma”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara wa leo umejikita katika kufafanua baadhi ya maneno yaliyopo kwenye ziara na dua mbalimbali”.

Idhaa ya Alkafeel ni ya kwanza hapa nchini kujikita katika kuelimisha mwanamke na kujenga familia mambo ambayo ndio msingi wa kujenga jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: