Makamo kiongozi mkuu wa kitivo Dokta Haitham Alghazali amesema “Punguzo hilo ni sehemu ya kuonyesha thamani ya kazi kubwa inayo fanywa na wauguzi na mchango mkubwa waliotoa wakati wa janga la korona”.
Akaongeza kuwa “Kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed kwa kushirikiana na sekta ya wauguzi, tunapokea watumishi wa wizara ya afya na watoto wao kwa punguzo la bei la asilimia Hamsini (%50) huku wahitimu wa kidato cha sita wakipunguziwa hadi asilimia themanini (%80)”.