Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kitafanya muhadhara kwa njia ya mtandao wenye anuani isemayo (Mbinu za kupambana na changamoto), utatolewa mubashara kupitia mtandao wa telegram.
Kiongozi wa kituo bibi Sara Hafaar amesema “Muhadhara utajikita katika kueleza changamoto na njia za utatuzi wake”.
Kwa mujibu wa maelezo ya Sara, kituo kinafanya kila kiwezalo katika kujenga uwelewa kwa familia na jamii ya wanawake, kwa ajili ya kujenga jamii bora.
Kumbuka kuwa muhadhara utatolewa Jumamosi ijayo (28/10/2023m) saa tano asubuhi.