Atabatu Abbasiyya inaomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Atabatu Abbasiyya imeomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza, kwa kufanya majlisi ya kuomboleza.

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya kundi kubwa la Mazuwaru wa malalo takatifu.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha akapanda kwenye mimbari Shekhe Ahmadi Swamiri.

Shekhe Swamiri ameongelea historia ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na dhulma alizofanyiwa baada ya kifo cha baba yake, na jinji alivyo pambana kutetea bendera ya Utume na Uimamu, alihami ujumbe wa baba yake na kutetea Uimamu wa mume wake (a.s).

Majlisi ikahitimishwa kwa qaswida na tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia ya huzuni na majonzi katika nyoyo za waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: