Atabatu Abbasiyya imefanya semina ya kuwajengea uwezo katika mambo tofauti watumishi wapya.
Sayyid Rasuul Twaaiy kutoka idara ya mahusiano ya ndani chini ya kitengo cha mahusiano amesema “Semina imesimamiwa na kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya na imedumu kwa muda wa siku tano, wamepewa uwelewa kuhusu nafani ya Ataba na mikakati yake sambamba na kujibu maswali kutoka kwao”.
Akaongeza kuwa “Semina ilikuwa na muhadhara kuhusu mambo ya utawali, mali, Dini na mahusiano, aidha watumishi wapya wamepewa maelezo kuhusu vitengo vya Ataba na miradi yake, wameambiwa mambo mbalimbali kuhusu Atabatu Abbasiyya na wakapewa nafasi ya kuuliza maswali”.
Kwa mujibu wa Twaaiy “Semina imejikita katika kuhimiza maadili mema kazini na kulinda heshima ya kila mtu”.