Maukibu imeanza matembezi yake ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba qaswida na tenzi za kuomboleza, zilizo amsha hisia ya huzuni na majonzi katika nyoyo za waumini na wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Baada ya kufika katika malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) wakafanya majlisi ya kuomboleza, zikasomwa tenzi na qaswida zilizotaja dhulma alizofanyiwa bibi Zaharaa (a.s).