Sayyid Swafi ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed na kumpongeza rais mpya wa chuo hicho.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed na kumpongeza rais mpya wa chuo hicho Dokta Judat Nuri Aljash’ami kwa kupewa madaraka hayo.

Katika ziara hiyo Sayyid Swafi amefuatana na Muheshimiwa rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Dida Mussawi, na kupokewa na rais wa chuo Dokta Judat Nuriy Aljash’ami, Dokta Maitham Hamidi Qambari, Dokta Alaa Mussawi na wakuu wa vitengo.

Sayyid Swafi ametoa pongezi kwa Dokta Judat Nuri Aljash’ami kwa kuteuliwa kuwa rais wa chuo hicho, akimpokea Dokta Maitham Hamidi Qambari aliyetumikia nafasi hiyo kabla yake.

Akasisitiza umuhimu wa kuendeleza sekta ya elimu, tafiti na malezi katika chuo, akahimiza zaidi sekta ya maelekezo ya nafsi na malezi kwani jambo hilo ni muhimu sana kwa wanafunzi wa chuo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: