Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha mtoto wa Mtume (s.a.w.w) mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s).
Majlisi imesimamiwa na wakuu wa chuo na kuhudhuriwa na watumishi, wakufunzi na wanafunzi.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikafuata ziara ya Fatuma Zaharaa (a.s), halafu muhadhara wa kielimu ukatolewa na Dokta Zainabu Alkhafaji wenye anuani isemayo (Ni nani bibi Fatuma Zaharaa -a.s?).
Baada ya Majlisi wanafunzi wakapewa nafasi ya kutembelea madarasa yatakayotumiwa na mabinti watakao shiriki kwenye hafla ya kutimiza umri wa kuwajibikiwa na sheria mwaka huu, ambapo watapewa nasaha kutoka katika usia wa bibi Zaharaa (a.s) kuhusu kujilinda, usafi na hijabu.