Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inafanya semina ya Nahjul-Balagha ambayo imehudhuriwa na walimu (110).
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Semina ya Nahjul-Balagha imehusisha wakufunzi wote wa Maahadi na matawi yake yaliyopo ndani na nje ya mji wa Karbala, semina hiyo inatokana na umuhimu wa kitabu hicho, kila mtu anatakiwa achote elimu iliyomo kwenye kitabu hicho”.
Akaongeza kuwa “Semina imepata muitikio mkubwa, kwani idadi ya washiriki imefika (110)”.
Maahadi inakawaida ya kutoa semina na warsha kwa watumishi wake, kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwafundisha mambo yatakayo wasaidia katika uhai wao.