Atabatu Abbasiyya imekamilisha maandalizi ya program ya kimtandao Multaqal-Kafeel awamu ya kwanza.
Program hiyo itaendeshwa katika ardhi ya chuo kikuu cha Al-Ameed na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na taasisi zinazohusika na mambo ya teknolojia, kwa ajili ya kuonyesha utendaji wa teknolojia katika uwanja wa kazi na kuonyesha program zinazosaidia jamii.
Program itadumu kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe (30/10 hadi 1/11/2023m), vitengo tofauti vya Ataba vitashiriki kwa kuonyesha uzowefu wao katika sekta ya teknolojia.
Program ya Multaqa itahusisha warsha na maonyesha mbalimbali, kwa lengo la kuonyesha maendeleo ya kiteknolojia yaliyopo duniani na mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo kupitia raia wa Iraq.