Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amekagua maendeleo ya shule za Al-Ameed na mikakati ya baadae ya kitengo cha malezi na elimu ya juu.
Amefanya hivyo kwa kutembelea shule zilizochini ya kitengo cha malezi na elimu katika Ataba tukufu, amepokewa na rais wa kitengo Dokta Hassan Daakhil na makamo wake Ustadh Yusufu Twaaiy, mkuu wa shule za wavulana za Al-Ameed Dokta Haidari A’raji na Ustadhat Mina Waaili.
Daakhil akasema “Ziara ya Muheshimiwa Sayyid Swafi ni kwa ajili ya kuangalia utendaji wa shule zetu na uendeshaji wa mafunzo ya kujengea uwezo idara zetu na kuboresha uwezo wa walimu wa shule za Al-Ameed”.
Akaongeza kuwa “Tumefanya maandalizi ya hafla ya wahitimu wa vyuo vikuu awamu ya sita, itakayo fanyika katika viwanja vya Shule za Al-Ameed za wasichana” akasema “Sayyid Swafi amebariki program hiyo na maandalizi yaliyofanywa na kitengo cha malezi na elimu ya juu”.