Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s).
Kikao hicho kimesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa.
Kiongozi wa harakati za Qur’ani katika Maahadi Dokta Ali Hamdi, amesema “Kikao hiki ni sehemu ya kufanyia kazi maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo (Kitabu kilicho barikiwa tumekiteremsha kwako ili watafakari aya zake), tunaonyesha mafundisho ya Qur’ani na kutafakari aya zake, sio kwa kiwango cha maneno na herufi tu, bali kwa kiwango cha kuzifahamu aya na kutafakari mafundisho yake”.
Akaongeza kuwa “Lengo la mradi huu ni kujenga uwelewa na aya za Qur’ani tukufu” akasema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani hufanywa maeneo tofauti, ikiwa ni pamoja na Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) siku zote za wiki na kuhudhuriwa na makundi ya watu tofauti wakiwemo wanajeshi”.