Kitengo cha miradi ya kihandisi kimejiandaa kushiriki kwenye kongamano la kiteknolojia Multaqal-Kafeel.

Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimejiandaa kushiriki kwenye kongamano la kiteknolojia Multaqal-Kafeel.

Kongamano litafanywa katika eneo la chuo cha Al-Ameed na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka taasisi tofauti za kiteknolojia, kongamano litadumu kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe (30/10/ hadi 1/ 11/2023m), kwa ushiriki wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya.

Kiongozi wa idara ya mawasiliano na teknolojia chini ya kitengo hicho Mhandisi Farasi Abbasi Hamza amesema “Idara imekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye kongamano la kiteknolojia Multaqal-Kafeel litakalo fanyika katika majengo ya chuo kikuu cha Al-Ameed”.

Akaongeza kuwa “Ushiriki wa idara yetu utahusisha kuonyesha matamko na mfumo wa kuhesabu mazuwaru kieloktronik, sambamba na kuonyesha shuhuda za ufanyaji kazi wa sekta ya teknolojia”.

Aendelea kusema “Washiriki wataandaliwa vifaa vyote vinavyohitajika kwenye kongamano, kama vile kompyuta, luninga, mfumo wa sauti na intaneti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: