Chuo kikuu cha Alkafeel kimejiandaa kuonyesha mfumo wa namba kwenye kongamano la kiteknolojia la Multaqal-Kafeel.

Chuo kikuu cha Alkafeel kimekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye kongamano la Multaqal-Kafeel, kupitia kuonyesha mfumo wa namba uliotengenezwa na watumishi wake.

Shughuli za kongamano zitafanywa katika chuo kikuu cha Al-Ameed na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe (30/10/ hadi 1/11/2023m).

Mkuu wa kituoa cha Alkafeel chini ya chuo kikuu Sayyid Saamir Swafi amesema “Kituo kimekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye kongamano la Multaqal-Kafeel, ambapo kitaonyesha shughuli tofauti zilizo anzishwa na kufanywa na watumishi wake”.

Akaongeza kuwa “Mifumo mingi itakayo onyeshwa inatumika katika vitengo vya Atabatu Abbasiyya na baadhi za wizara, kama vile wizara ya malezi na elimu ya juu pamoja na taasisi za kiserikali na kiraia”.

Vitengo kadhaa vya Atabatu Abbasiyya vitashiriki kwenye shughuli za kongamano, kwa kuonyesha uzowefu wake katika mambo ya teknolojia na mitandao ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: