Chuo kikuu cha Al-Ameed kimekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye kongamano la Multaqal-Kafeel la kiteknolojia

Chuo kikuu cha Al-Ameed kimekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye kongamano la Multaqal-Kafeel linalo ratibiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Muwakilishi wa kitengo cha kompyuta Dokta Bariri Atwari amesema “Kitengo kimekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye kongamano kupitia program tofauti zilizo tengenezwa na watumishi wa kitengo hicho”.

Akaongeza kuwa “Ushiriki wetu utahusisha kuonyesha mafanikio ya kitengo katika program zake za kiteknolojia na taaluma, huduma za kimalezi na kielimu, mafungamano ya mwanafunzi na mwalimu, pamoja na program zinazotumika kwenye mfumo wa serikali na mashirika ya kiraia”.

Kongamano litafanyika katika eneo la chuo kikuu cha Al-Ameed kuanzia tarehe (30/10/ hadi 1/11/2023m), kwa ushiriki wa vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya, vitakavyo onyesha uzowefu wake katika mambo ya kiteknolojia na mitandao ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: