Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinatambulisha huduma za kimtandao zinazotolewa na Maahadi ya turathi za Mitume, kupitia ushiriki wake kwenye kongamano la Multaqal-Kafeel.
Kongamano linafanywa kwenye ardhi ya chuo kikuu cha Al-Ameed kuanzia tarehe (30/10/ hadi 1/11/2023m) kwa ushiriki wa vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya, ambavyo vitaonyesha uzowefu wao katika mambo ya teknolojia na mitandao ya kijamii.
Kiongozi wa idara ya ufundi katika Maahadi Sayyid Amaar Wahabi Razaaq amesema “Ushiriki wetu unahusisha kutambulisha huduma za kimtandao zinazotolewa na Maahadi ya turathi za Mitume”.
Akaongeza kuwa “Miongoni mwa huduma zinazotolewa ni, Hauza ya elimu masafa, app za simu ganja za kisasa kwa mfano App ya Ajwibatul-Muyassarah, Marjaa-Aqaaidiy, App ya Swalihina na zinginezo”.